Tuesday, July 17, 2012

CHEGE AMGONGA MWENDESHA PIKIPIKI, AMVUNJA MGUU

Chegge Chigunda

Na Mwandishi Wetu
MSANII wa kundi la TMK Wanaume Family, Chegge, amehusika katika ajali iliyohusisha gari yake na pikipiki usiku huu na kusababisha uvumi kwamba muimbaji huyo wa 'single' ya 'Mwanayumba' amepoteza maisha.


Kwa mujibu wa mahojiano baina ya mtangazaji Diva Loveness Luv wa kipindi cha Ala za Roho cha Clouds FM na muimbaji huyo, ajali hiyo imetokea katika barabara ya Mbozi, Temeke na kwamba Chegge yuko salama na wenzake wote isipokuwa dereva wa pikipiki amejeruhiwa vibaya baada ya kuvunjika mguu.


Wakati akiongea kwa simu na Diva, Chege alisema: "Nimetokea Mombasa saa 12:00 jioni na kesho saa 2:00 asubuhi naelekea Kigoma kwenye shoo (na kundi la Kigoma All Stars)."


Alisema akiwa katika speed 60, akatokea mwenye pikipiki akiwa amelewa, akajaribu kumkwepa lakini wapi, akamgonga. Mwenye pikipiki ameumia vibaya, pikipiki ya jamaa huyo na gari yake pia vimeharibika vibaya pia.

"Ajali hii imetokea mida ya saa 4:00 usiku, pikipiki ya jamaa na gari yangu ni off kabisa... mie mkanda umeniokoa. Nimeenda hospitali, nikatibiwa na kuruhusiwa. Nashukuru kwamba niko poa, ila bega la kushoto nd'o kidogo linanisumbua," Chegge alieleza zaidi.   

No comments:

Post a Comment