Saturday, July 14, 2012

BRIGITA ALFRED NDIYE MISS SINZA 2012

MARIA JOHN ATWAA TAJI LA SUFIANIMAFOTO MISS TALENT

Miss Sinza 2012, Brigita Alfred (katikati) akipunga mkono kwa furaha akiwa na washindi wenzake, mshindi wa pili Judith Sangu (kushoto) na watatu Esther Mussa baada ya kutangazwa washindi katika shindano hilo lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi wa Mawela Social, Sinza Jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Kampuni ya SPM-Sufiani Photo Magic na Mtandao wa Sufianimafoto.blogspot.com, Nasma Sufiani, akimvisha taji na kumkabidhi zawadi Maria John baada ya kuibuka kidedea katika shindano la kumsaka mshindi wa taji dogo la Sufianimafoto Miss Talent lililofanyika ndani ya shindano hilo la Miss Sinza katika Ukumbi wa Mawela Social, Sinza jijini Dar es Salaam.
Sufianimafoto Miss Talent, Maria John akiwa na furaha baada ya kuvishwa taji hilo na kukabidhiwa zawadi yake.

 Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga (wa pili kulia) akiwa na baadhi ya wanakamati wakishuhudia shindano hilo.

 Mshiriki Nancy akipita jukwaani na vazi la ufukweni.
Mshiriki Naima Mohamed  akipita jukwaani na vazi la ufukweni. 
 Mshiriki Maria John akipita jukwaani na vazi la ubunifu.
 Msanii wa vichekesho wa kikundi cha Ze Comedy cha ITV, Massawe Mtata, ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Uongo Kweli, akishambulia jukwaa, wakati wa onyesho hilo na kuwapagawisha vilivyo, mashabiki wa fani ya urembo waliokuwapo ukumbini hapo.
 Mshiriki, Mariam Miraji, akipita jukwaani na vazi la ufukweni.
 Sehemu ya watu waliojitokeza kushuhudia shindano hilo.
 Madj wa Sufianimafo, wakiwa katika mitambo ya Sufianimafoto, iliyokuwa ikitumika katika shindano hilo, wakiendesha shughuli nzima ukumbini hapo.
 Pozi la Masawe Mtata kabla hajapanda jukwaani huku akiwa ameketi na akinadada ambao baadhi yao baada ya kushuka jukwaani walianza kumshabikia, ''he kumbe tumekaa na Masawe hapa hatujui, hebu nipe namba yako'', alisikika mmoja wao akisema, huku mwingine akisikika kumpiga mkwara Masawe, ''Ole wako umpe namba huyo dada ntakupasua'' alisema mwingine kana kwamba yeye alikuwa tayari amekwishawini kupata namba ya mchekeshaji huyo Ze Comedy ya ITV.
 Waimbaji wa Twanga Pepeta, wakishambulia jukwaa.
 Wanenguani na waimbaji wa Twanga, wakishambulia jukwaa.
 Mshiriki, Mariam, akipita jukwaani na vazi la usiku.
 Mshiriki, Maria John, akipita jukwaani na vazi la usiku.
 Mshiriki, Ester Mussa, akipita jukwaani na vazi la usiku.
 Warembo hao wakicheza shoo ya pamoja ya ufunguzi.
 Sehemu ya watu waliojitokeza kushuhudia shindano hilo.
 Masawe Mtata, akikamua jukwaani kibao chake cha Uongo Kweli.
 Miss Sinza 2011, (kushoto) akipozi na wenzake ukumbini hapo.
 Warembo waliofanikiwa kuingia hatua ya Tano Bora, wakipozi kwa picha, kutoka (kulia) ni Brigita Alfred, Judith Sangu, Nahma Said, Ester Mussa na Mariam Miraji, baada ya kutangazwa kutinga hatua hiyo.
Mshiriki Naima Mohamed akicheza kushindania taji la Sufianimafoto Miss Talent lakini bahati haikuwa yake.
Sufianimafoto Miss Talent, Maria John, akionyesha umahiri wake wakati akiwania taji hilo kwa kucheza wimbo mpya wa Tunda Man.
Mwalimu wa warembo hao, Mwajabu Juma, akipita jukwaani kusalimia wadau wa urembo.
Warembo wakicheza shoo ya pamoja ya ufunguzi.

Mshiriki Naima Mohamed akipita jukwaani na vazi la ubunifu
.
Mshiriki Ester Mussa akipita jukwaani na vazi la ubunifu.
Mshiriki Mariam akipita jukwaani na vazi la ufukweni.
.
Miss Sinza 2012, Brigita Alfred akipita jukwaani na vazi la ufukweni.

Na Mwandishi Wetu
MREMBO Brigita Alfred usiku wa kuamkia jana alitwaa taji la Redds Miss Sinza baada ya kuwashinda wenzake 13 katika kinyang’anyiro kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mawela Social Hall (Ten Star Lounge).

Tangu mwanzoni Brigita alionyesha dalili za kuja kuibuka mshindi kwa jinsi alivyouteka umati wa mashabiki wa urembo katika mashindano hayo yaliyodhaminiwa na kinywaji cha Redds, Dodoma Wine, Lady Pepeta, Flexi P, Jackz Cosmetics, Clouds FM, sufianimafoto.blogspot.com na Screen Masters.

Kwa ushindi huo, Brigita alipewa Sh. 500,000 na tiketi ya kuiwakilisha Sinza katika mashindano ya Redds Miss Kinondoni.

Mshindi wa pili katika kinyang’anyro hicho alikuwa Judith Sangu aliyezawadiwa Sh. 400,000 na mshindi wa tatu Esther Mussa alizawadiwa Sh. 300,000.

Mariam Miraji alishinda nafasi ya nne wakati ya tano ilikwenda kwa Nahma Saidi. Warembo wote hao watano walipata tiketi ya kushindana katika mashindano ya Miss Kinondoni.

Warembo wengine waliobaki, Naima Mohamed, Lulu Ambonela, Maria John,  Eva Mushi, Vailet John, Christina Samwel, Aisha Ramadhan, Nancy Musharuzi na Merina Mushi walipewa  zawadi ya kifuta jasho cha Sh. 100,000 kila mmoja katika shindano hilo lililopambwa na bendi ya African Stars wana Twanga Pepeta.


CHANZO: Sufianimafoto.blogspot.com

No comments:

Post a Comment