Wednesday, July 11, 2012

BREAKING NEWS: MELI YENYE MALI ZA TANESCO YAENDELEA KUTEKETEA KWA MOTO KISIWANI MAFIA

Mkurugenzi wa TANESCO, Eng. Mhando

Habari zilizofika punde na kuripotiwa pia katika Televisheni ya Taifa (TBC1) zinasema kuwa Meli ya Sahara II inaendelea kuteketea kwa moto baada ya kufika Mafia ikitokea jijini Dar na mizigo ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Kamanda wa wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ernest Mangu amekaririwa akisema kuwa jitihada za kuzima moto huo bado zinaendelea.

Imeelezwa zaidi kuwa Wilaya ya Mafia haina gari la zimamoto, hivyo wananchi wanendelea kufanya jitihada za kuzima moto huo kwa kutumia mikono na maji.
  

No comments:

Post a Comment