Saturday, July 7, 2012

BARCELONA WANAHITAJI MTU KAMA CROUCH

Jordi Alba akiwa katika "uzi" mpya wa Barca utakaovaliwa msimu ujao.
Na urefu wote huo bado anamfikia begani kudadadeki...... Peter Crouch (kushoto) wa Stoke City akimiliki mpira huku akichungwa na Anton Ferdinand (kulia) wa QPR wakati wa mechi ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Loftus Road Mei 6, 2012 mjini London, England.

BEKI wa zamani wa Barcelona, Chapi Ferrer amehoji kuhusu maamuzi ya kumsajili nyota wa zamani wa Valencia, Jordi Alba.

Ferrer, ambaye pia aliwahi kuichezea Chelsea, anaamini kwamba udhaifu wa Barca haujapatiwa ufumbuzi kwa kumnunua beki mfupi.

"Ni beki mzuri anayetawala kila mahala uwanjani, ana kasi na ni mjanja sana," Ferrer alisema. "Ataifanya timu iwe na mizani sawa, kwa sababu ataleta uhai katika upande wa kushoto.

"Kufikia sasa Barcelona inashambulia zaidi kwa kutegemea upande wa kulia wa Daniel Alves, kwa sababu si [Eric] Abidal wala Adriano aliyeweza kuwa tishio akipanda mbele kama ilivyo upande wa kulia.

"Lakini kuna tatizo la urefu. Watapata shida ya kupiga krosi, 'fri-kiki' na kona, kwa sababu wachezaji wao warefu pekee watakuwa ni mabeki wawili wa kati na Sergio Busquets, lakini hiyo ndiyo staili ya kucheza ya Barca.

"Timu inatumia muda mwingi katika kushambulia na wanahitaji wachezaji wenye kasi ambao wanaweza kuchana safu za mabeki. Kwa kusema hivyo, kama mabeki wa pembeni wote watakuwa wamepanda mbele, waliobaki itabidi wakae nyuma kulinda."

Licha ya kushambulia mfululizo na kutumia muda mrefu wa mechi wakiwa ndani ya boksi la wapinzani dhidi ya timu "zinazopaki basi", wachezaji wa Barcelona wamekuwa wakilazimika kurudisha mipira nyuma kwa sababu hawana wachezaji wa kucheza krosi za juu. Bila ya shaka Peter Crouch atawafaa na atakuwa mfungaji bora.

No comments:

Post a Comment