Hapa Balotelli anatembea 'zero distance' kabla ya kuzinguana na Rafaella |
Balotelli na Rafaella |
Twende mpenzi...! Balotelli akiwa na Rafaella enzi hizo wakiwa na mapenzi ya kugandana kama luba. |
Haa..haa...haaaa...pendeza eeee! |
Balotelli na mpenzi wake wa zamani, Rafaella |
Balotelli na Rafaella wakikatiza mitaa baada ya kutoka 'shopping' kabla hawajamwagana |
Hapa ni enzi za mapenzi motomoto kati ya Balotelli na Rafaella |
MILAN,
Italia
MARIO
Balotelli anataka achukuliwe vipimo vya vinasaba (DNA) baada ya mwanamke wa
Kiitaliano, Raffaella Fico kudai jana kwamba ana mimba ya straika huyo wa
klabu ya Manchester City.
Raffaella
ambaye ni mpenzi wa zamani wa mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Italia,
aliliambia jarida la Chi kwamba alimpa Balotelli taarifa za ujauzito wake
Alhamisi baada ya mechi yao ya nusu fainali ya Euro 2012 dhidi ya Ujerumani,
akimueleza zaidi kuwa ana mimba yake ya miezi minne.
Balotelli
sasa ametoa taarifa kwa vyombo vya habari inayodai kwamba hakusudii kukwepa
majukumu, lakini anataka wachukuliwe vipimo vya DNA kuthibitisha kama kweli
yeye ndiye baba wa mtoto huyo.
"Ingawa
sipendi kuzungumzia mambo yangu binafasi hadharani, nafikiri katika hili nina
wajibu wa kuweka wazi, kwa mara ya kwanza na ya mwisho, kuhusiana na mahusiano
yangu na Raffaella Fico," straika huyo mwenye miaka 21 alieleza.
"Uhusiano
wetu ulifikia ukomo mwanzoni mwa Aprili na tangu wakati huo hatujaonana, wala
kuwasiliana.
"Sina
chochote cha kufuatilia maisha yake na Raffaella hana cha kufuatilia juu ya
maisha yangu.
"Raffaella
anatambua vyema kwamba tangu tulipoachana, sikuwa na sina nia ya kurudiana
naye.
"Lakini
kwa sababu ya kile kilichokuwapo kati yetu, sikutaka kuzungumzia suala hili,
hata pale pale palipokuwa na vitu vya uongo vilivyokuwa vikisemwa na kaundikwa
kuhusiana na hili.
"Siku
chache zilizopita nilijulishwa na watu wengine kwamba Raffaella ana mimba. Kwa
sababu hii, niliamua kuwasiliana naye na baada ya kumuuliza ndipo
aliponithibitishia kuwa ni kweli.
"Nimehuzunishwa
sana. Sidhani kama ni kawaida kutojulishwa hadi kufikia mwezi wa nne (kuhusiana
na mimba).
"Sielewi
ni kwanini hakuniambia mapema jambo kubwa kama hili.
"Nitabeba
majukumu yote wakati nitakapokuwa na ushahidi kwamba kweli ana mimba yangu."
Balotelli
aliendelea: "Vilevile, inanikera kuona kwamba tayari ameshaanza kusaka
fedha kwa kuuza mahojiano yake juu ya habari hii na picha.
"Nadhani
kwamba Rafaella tayari ameshakuwa maarufu na hivyo hahitaji kutumia habari hii
kwa lengo la kujitangaza.
"Hii
ni mara ya kwanza na ya mwisho kwangu kuzungumzia suala hili hadharani na hivyo
sikusudii kujibu chochote kuhusiana na kile kinachosemwa au kuandikwa na
Raffaella."
Fico
amedai kwamba Balotelli, aliyefunga mara mbili na kuisaidia Italia kuibuka na
ushindi wa 2-1 dhidi ya Ujerumani, alijawa na furaha kusikia kwamba anatarajia
kupata mtoto.
No comments:
Post a Comment