Thursday, July 12, 2012

AMIR KHAN ARUDISHIWA MKANDA WAKE WBA

Amir Khan

AMIR Khan amerejeshewa mkanda wake wa WBA wa 'light-welterweight' na bodi inayosimamia mchezo huo na atauvaa wakati atakapopambana na bingwa wa WBC, Danny Garcia mjini Las Vegas Jumamosi.

Muingereza huyo alipoteza mataji yake ya WBA na IBF kwa Lamont Peterson Desemba mwaka jana katika mazingira ya kutatanisha.

Mechi ya marudiano iliyopangwa ilifutwa baada ya Peterson kubainika anatumia dawa zinazokatazwa michezoni.

"Haki imetendeka," Khan alisema. "Inamaanisha pambano langu hili  (dhidi ya Garcia) litaonyesha ni nani bora katika uzani huu."

Khan alikata rufaa kufuatia kupigwa kwa pointi na Peterson, huku WBA ikisema kulikuwa na mambo "yasiyo ya kawaida" katika pambano lao.

Bondia huyo mzaliwa wa Bolton alisema: "Nina furaha kwamba WBA wamenirejeshea ubingwa wangu; inamaanisha naingia katika pambano hili kama bingwa wa dunia.

"Kuna nafasi ya kushinda taji la WBC pia lakini si hilo tu, heshima ya mkali wa kweli wa uzito huu inakuja.

"Kuna mataji makubwa matano katika uzito huu na kama nitashinda taji hili, nitakuwa nimeshatwaa mataji manne kati ya hati.

"Taji pekee ambalo sijawahi kutwaa ni la WBO, lakini nilijaribu kupambana na Tim Bradley kuliwania akakataa.


"Kama nitashinda dhidi ya Garcia, itamaanisha kwamba nimeshafanya kila kitu ninachotaka katika uzani huu."

Linaongeza umuhimu zaidi katika pambano lake la
'light-welterweight' dhidi ya Garcia, ambalo Khan alidai linalifunika kirahisi kiumuhimu pambano la uzito wa juu baina ya David Haye na Dereck Chisora litakalofanyika mjini London usiku huo huo wa Jumamosi.

No comments:

Post a Comment