Saturday, June 23, 2012

RONALDO NI WA SAYARI NYINGINE - PEPE

Pepe (kushoto) wa Ureno akishangilia pamoja na wachezaji wenzake Cristiano Ronaldo (katikati) na Nani wakati wa mechi yao ya Kundi B la UEFA Euro 2012 dhidi ya Uholanzi kwenye Uwanja wa Metalist Juni 17, 2012 mjini Kharkov, Ukraine.

BEKI wa Real Madrid, Pepe amemsifu mchezaji mwenzake Cristiano Ronaldo baada ya kufunga bao la ushindi la Ureno dhidi ya Jamhuri ya Czech.

Goli la kichwa la Ronaldo liliipeleka Ureno kwenye nusu-fainali ya Euro2012.

"Kwa kadri mnavyomsema zaidi Cristiano Ronaldo, ndivyo anavyozidi kuwa mkali. Yeye ni mchezaji kutoka sayari nyingine. Kwake, kuwa mwanasoka bora duniani kunamaanisha mataji. Yuko juu sana," Pepe aliiambia RTP.

"Uwanjani, namuangalia na kufikiria yeye ni mchezaji kutoka sayari nyingine. Huwa anayapiku aliyoyafanya mwenyewe zamani kila siku."

No comments:

Post a Comment