Wednesday, June 27, 2012

Pirlo: Sistahili tuzo ya Ballon d'Or

Andrea Pirlo wa Italia akifunga penalti kwa kuudokoa mpira wakati wa hatua ya kupigiana “matuta” dhidi ya England katika robo fainali ya michuano ya Euro 2012 kwenye Uwanja wa Olympic Juni 24, 2012 mjini Kiev, Ukraine.

Andrea Pirlo wa Italia akifunga penalti kwa kuudokoa mpira dhidi ya kipa Joe Hart wa England wakati wa hatua ya kupigiana “matuta” katika robo fainali ya michuano ya Euro 2012 kwenye Uwanja wa Olympic Juni 24, 2012 mjini Kiev, Ukraine.

ANDREA Pirlo, ambaye ameng'aa soka la dunia kutokana na utawala wake katika Euro 2012, haamini kama anastahi kutwaa tuzo ya FIFA Ballon d'Or mwaka huu kwa sababu hajafunga magoli ya kutosha.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 33, ambaye timu yake ya Italia leo usiku itaikabili Ujerumani katika nusu fainali ya Euro 2012, hajawahi kuwa mfungaji sana kutokea katika nafasi yake ya nyuma ya kiungo lakini ameacha gumzo katika michuano hicho kutokana na penalti yake ya kudokoa wakati wa kupigiana "matuta" katika mechi ya robo fainali dhidi ya England.

Alipoulizwa kama anadhani anastahili kutajwa mshindi wa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia wa Mwaka baada ya pia kuiongoza Juventus kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Italia (Serie A) mwezi Mei, mshindi huyo wa Kombe la Dunia 2006 alikataa.

"Hapana, kuna (Lionel) Messi na (Cristiano) Ronaldo. Ni jambo lisilowezekana kuwa mbele yao," aliuambia mkutano na waandishi wa habari uliowahusisha wanahabari kutoka nchi mbali kama Marekani na China.

"Wao wamefunga magoli mengi sana. Sidhani kama naweza hata kujadiliwa."

------------

No comments:

Post a Comment