Monday, June 25, 2012

MANCINI AFICHUA KINACHOIPONZA ENGLAND

Roberto Mancini

KOCHA wa Manchester City, Roberto Mancini anaamini kwamba England haitatwaa ubingwa katika michuano yoyote ya kimataifa hadi hapo itakapokubali kubadili ratiba yake ya sasa ya ligi kuu na kuruhusu mapumziko ya majira ya baridi.

Muitalia huyo alisisitiza kwamba uchovu wa safari ndefu ya msimu wa Ligi Kuu ya England ndio sababu kubwa ya kutolewa kwao kwa ‘matuta’ na Italia katika robo fainali ya Euro 2012 jana.
""Fabio Capello ameifanyia makubwa England," aliiambia Rai Radio 2. 

"Na kama angekuwapo katika benchi la ufundi, bado Italia ingelazimika kufanya kazi ya ziada."
"Nadhani wachezaji wa England wanalipa gharama itokanayo na ukweli kwamba wamekuwa wakicheza bila kupumzika kwa miezi 10 mfululizo.

"Baadaye wanafika kwenye mashindano wakiwa taaban. Siku zote wao hushambulia, sio kuzuia tu kama ilivyokuwa katika michuano hii ya Ulaya."

No comments:

Post a Comment