Sunday, June 24, 2012

NASRI AMKERA BLANC KWA KUTUKANA WAANDISHI

Kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa, Laurent Blanc (kushoto) akishikana mikono na Samir Nasri baada ya kipigo cha 2-0 walichokipata kutoka kwa Hispania katika mechi yao ya robo fainali ya Euro 2012 kwenye Uwanja wa Donbass Arena mjini Donetsk

LUGHA chafu iliyotolewa na Samir Nasri dhidi ya mwandishi wa habari kufuatia kipigo cha Ufaransa cha 2-0 kutoka kwa Hispania katika mechi yao ya robo fainali ya Euro 2012 Jumamosi ilikuwa ni "mbaya, mbaya mno" kwa sifa yake, kocha Laurent Blanc amesema. 


"Ni jambo la kujutia lakini ni matatizo binafsi baina ya Samir na vyombo vya habari. Ni mbaya, mbaya sana kwa sifa yake lakini jambo hili linapofanywa wakati yuko katika timu ya Ufaransa ni mbaya kwa sifa ya timu," Blanc alikiambia kituo cha televisheni cha TF1 cha Ufaransa jana. 

"Kwa mujibu wa ninachofahamu, alikosa heshima kwa mwandishi ambaye pia kwa wakati fulani alimkosea heshima Nasri." 

Kiungo Nasri tayari alihusika katika majibizano na vyombo vya habari katika michuano hiyo wakati alipoonyesha ishara ya "funga domo" baada ya kufunga goli la kusawazisha la Ufaransa katika sare ya 1-1 dhidi ya England katika mechi yao ya ufunguzi. 

"Nilimweleza nilichofikiria kuhusu jambo hili (baada ya tukio la kwanza) lakini naona ujumbe haukumuingia," aliongeza Blanc.

No comments:

Post a Comment