Friday, June 22, 2012

LeBRON JAMES AIPA MIAMI HEAT UBINGWA NBA

*Mwenyewe atwaa tuzo ya MVP

LeBron James akishangilia baada ya kuisaidia Miami Heat kutwaa ubingwa wa ligi ya kikapu ya NBA

MIAMI, Marekani
LeBRON James ndiye mshindi wa tuzo ya MVP wa fainali ya ligi ya kikapu ya NBA hapa Marekani.

James alimaliza akiwa amefunga "triple double" yaani pointi 26, akitoa pasi 13 za kufunga na pia akiwahi ribaundi 11 katika Game 5 ya mfululizo wa mechi saba za fainali ya ligi ya kikapu Alhamisi usiku, na kuiongoza Miami Heat kuibuka na ushindi mnono wa pointi 121-106 dhidi ya Oklahoma City Thunder.

Miami imetwaa ubingwa wa pili katika historia ya michuano hiyo mikubwa, na James ameibuka mshindi kwa mara ya kwanza katika fainali tatu alizocheza.

James na timu yake ya zamani ya Cleveland Cavaliers ilifungwa katika fainali dhidi ya San Antonio Spurs mwaka 2007, kisha akiwa na timu ya Miama Heat walifungwa katika Game 6 dhidi ya Dallas Mavericks msimu uliopita.

Alipoulizwa jana kwamba taji hilo linamaanisha nini kwake, James alisema: "Linamaanisha kila kitu."

Baada ya matokeo ya 1-1 katika mechi mbili za kwanza za mfululizo wa mechi saba za fainali msimu huu, Oklahoma City Thunder walidhaniwa wangeleta ushindani mkubwa dhidi ya Miami.

Lakini walikumbana na vipigo vitatu mfululizo na kuangukia nyuma 4-1 na hivyo kutokuwepo tena umuhimu wa kumalizia mechi mbili zilizobaki katika mfululizo wa mechi saba za fainali.

-------------------

No comments:

Post a Comment